Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 15:46

Besigye azuiliwa katika gereza la Luzira


Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, akiwa amekamatwa na polisi
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, akiwa amekamatwa na polisi

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dr. Kiiza Besigye amefunguliwa mashtaka ya uhalifu kwa kuitisha maandamano ya kupinga kupanda kwa bei za bidhaa muhimu na kutaka serikali kuingilia kati na kudhibithi ongezeko hilo.

Besigye, ambaye amewania uraia mara nne nchini Uganda, alikamatwa jana jumanne na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Nagalama. Mashariki mwa Kampala.

Alikamatwa baada ya kuwahepa polisi waliokuwa wamekita kambi nyumbani kwake kuhakikisha kwamba asitoke nyumbani, kwa mda wa karibu wiki tatu.

Kabla ya kukamatwa, alihutubia watu katikati kwa Kampala, akisema kwamba “ni lazima serikali ya rais Yoweri Museveni ihakikishe kwamba inatoa ushsuru kwa bidhaa muhimu ili kuwezesha raia kuzinunua kwa bei nafuu.”

Mwendesha mashtaka wa serikali amesema mahakamai kwamba “hatua ya Besigye kuitisha maandamano inalenga kusababisha uharibifu wa mali.”

Mahakama imeagiza kwamba azuiliwe katika gereza la Luzira, baada ya kukataa kulipa kiasi cha shilingi za Uganda milioni 30 ili awachiliwe kwa dhamana.

Besigye amesema kwamba “ni heri niishi gerezani kuliko kulipa kiasi hicho cha pesa,”akiongezea kwamba dhuluma ambazo ametendewa kwa kuzuiliwa nyumbani kwake licha ya kuwepo amri ya mahakama kuwazuia polisi kufanya hivyo, Pamoja na kiasi cha pesa ambacho kimeitishwa na mahakama, vyote ni uvunjaji wa sheria.

XS
SM
MD
LG