Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:24

Besigye amekamatwa na kuzuiliwa kwa gari la polisi


Mwanaharakati wa kisiasa Dr. Kiiza Besigye akikamatwa na maafisa wa polisi
Mwanaharakati wa kisiasa Dr. Kiiza Besigye akikamatwa na maafisa wa polisi

Mwanaharakati wa kisiasa nchini Uganda Dr. Kiiza Besigye amekamatwa alipokuwa anajaribu kutoka nyumbani kwake, na kuzuiliwa katika gari la polisi.

Besigye alikuwa anatoka nyumbani kwake, kuongoza maandamano ya kupinga kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu nchini Uganda.

Polisi wamezingira nyumba ya Besigye kwa wiki kadhaa, kuhakikisha kwamba hafiki katikati mwa jiji la Kampala.

“Sitakubali kuendelea kuzuiliwa nyumbani kwangu kama mfungwa, katika nchi yangu. Hili lazima lifike kikomo,” Amesema Besigye.

Polisi hawajasema sababu zilizopelekea kukamatwa kwa Besigye.

Besigye amekosoa utawala wa rais Yoweri Museveni kwa kile ametaja kama kutocchukua hatua kupunguza bei za bidhaa muhimu.

XS
SM
MD
LG