Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 10:28

Besigye aachiwa huru


Aliyekuwa mgombezi wa urais kwa kutumia tiketi ya chama cha FDC, Dkt Kiiza Besigye, sasa yuko huru baada ya kuzuiliwa nyumbani kwake kwa siku 41.

Polisi wameondoka nyumbani kwake Besigye baada ya amri ya mkuu wa polisi Generali Kale Kayihura, muda mfupi kabla ya mahakama kuu kuanza kusikiliza ombi la Besigye kutaka polisi kuondoka kwake.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:40 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakati hayo yakitokea mahakama kuu ya Uganda, ilisisitiza kwamba rais Yoweri Museveni ndie mshindi kwenye uchaguzi wa kitaifa uliofanyika Februari 18.

Mahakama hiyo imetupilia mbali rufaa iliokatwa na aliekuwa waziri mkuu na mpinzani wa Museveni, Amama Mbabazi.

Tume ya uchaguzi ilimtangaza Museveni kuwa mshindi tarehe 20 Februari kwa kujipatia asilimia 60 ya kura akifuatiwa na Kizza Besigye aliepata asilimia 30.5 ya kura zilizopigwa.

XS
SM
MD
LG