Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 07:15

Bensouda aelekea Rift Valley kwa upelelezi zaidi


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda
Mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, Fatou Bensouda, amekamilisha mazungumzo yake nchini Kenya na Rais wa nchi hiyo Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga, Jaji Mkuu pamoja na viongozi wengine wa juu katika serikali ya mpito.

Bi, Bensouda pia alianza kuchukua maoni Jumatano ya waathirika wa ghasia na mauaji yaliyotokea katika uchaguzi mkuu uliopita nchini humo kabla ya kuelekea katika miji ya Naivasha, Nakuru na Eldoret katika jimbo la Rift Valley ili kukutana ana kwa ana na baadhi ya waathirika wa ghasia hizo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:24 0:00
Kiungo cha moja kwa mojaRipoti zilizopatikana kufuatia mikutano yake na viongozi wa vyeo vya juu nchini humo zinasema bi, Bensouda alitilia mkazo umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na mahakama ya ICC ili kuwezesha mahakama hiyo kupata maelezo muhimu ya kuwezesha maafisa wa idara yake kutekeleza mashitaka hayo bila ya vikwazo.

Kiongozi huyo kutoka ICC pia amekuwa akitaka maelezo zaidi kuhusu akaunti za benki za washukiwa wanne mashuhuri nchini humo ambao wamefikishwa katika mahakama ya ICC kwa tuhuma za kuhusika na ghasia za uchaguzi mkuu uliopita ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 na wananchi wengi kukoseshwa makazi ndani ya nchi.

Pia alidai kuwa baadhi ya mashahidi katika kesi ya washukiwa hao wanafanyiwa vitisho na baadhi yao wameanza kubadili ushahidi waliokusudia kuutoa mahakamani.

Tangu kesi za washukiwa hao kuwasilishwa huko The Hague kumekuwepo na taarifa kutoka mjini Nairobi kwamba uhusiano kati ya serikali ya Kenya na mahakama ya ICC sio mzuri.
XS
SM
MD
LG