Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:50

Benki ya Dunia yapata mkuu mpya


Mkuu mpya wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim mjini Washington
Mkuu mpya wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim mjini Washington

Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria na Jose Antonio Ocampo wa Colombia pia walikuwa katika kinyang'anyiro

Wakurugenzi wakuu wa Benki ya Dunia Jumatatu wamemchagua Mmarekani Jim Yong Kim kuwa mkuu mpya wa taasisi hiyo ya maendeleo ya kimataifa. Dr. Kim aliyeteuliwa na Rais Barack Obama wiki chache zilizopita ni daktari na mtaalam wa mambo ya kale ambaye alikuwa rais wa chuo kikuu cha Dartmouth hapa Marekani.

Miongoni mwa kazi zake za nyuma aliwahi kuongoza juhudi za Umoja wa Mataifa kupambana na UKIMWI, aliunda asasi isiyo ya kiserikali kukuza upatikanaji wa huduma za afya katika nchi masikini, pia alifundisha katika chuo kikuu maarufu Marekani - Havard. Dr. Kim ataongoza Benki ya Dunia kwa kipindi cha miaka mitano akichukua nafasi ya Robert Zoellick ambaye muhula wake ulimalizika mwezi Juni.

Chini ya makubaliano yasiyo rasmi Mmarekani siku zote amekuwa akiongoza Benki ya Dunia na raia wa Ulaya akiongozi Shirika la Fedha Duniani - IMF. Wakosoaji wanasema makubaliano hayo yamepitwa na wakati.

Mwaka huu, kwa mara ya kwanza, kulikuwa na washindani katika nafasi hiyo. Waziri wa Fedha wa Nigeria Ngozi Okonko-Iweala, na waziri wa fedha wa Colombia ambaye pia ni mtaalam wa maendeleo Jose Antonio Ocampo pia walikuwa wanawania nafasi hiyo.

XS
SM
MD
LG