Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:16

Kiongozi wa upinzani Uganda akamatwa


Dr. Kizza Besigye akizungumza na waandishi
Dr. Kizza Besigye akizungumza na waandishi

Kiongozi wa upinzani ambaye ni mgombea urais nchini Uganda Kizza Besigye ametiwa nguvuni leo Alhamisi akiwa anarudi nyumbani kwake Kampala baada ya kutoka kupiga kura.

Waandishi Kampala wanasema Besigye anashikiliwa katika kituo cha polisi kilichopo karibu na nyumabani kwake mjini Kampala.

Besigye alipiga kura katika eneo la kijijini kwao na alikuwa akirudi nyumbani kwao mjini Kampala alipotiwa nguvuni na polisi kabla hajafika nyumbani kwake.

XS
SM
MD
LG