Wakazi kutoka kwenye maeneo yaliyoathiriwa zaidi wameshauriwa kufanyia kazi nyumbani wakati barabara kadhaa pamoja na bustani zilkifungwa katika mji huo wenye takriban wakazi milioni 22.
Mlipuko wa sasa unasemekana kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu kesi ya kwanza kugundulika mwaka 2020. Usafiri wa mabasi umesitishwa kwenye baadhi ya vitongoji kama vile Chaoyang na Fangshan ambavyo vinasemekana kuathiriwa zaidi. Kesi mpya 49 zimeripotiwa Jumapili na hivyo kufikisha jumla ya maambukizi mapya tangu Aprili 22 kufikia zaidi ya 760.