Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 11:42

Bashir ahudhuria mkutano wa IGAD


Bashir ahudhuria mkutano wa IGAD

Rais wa Sudan Omar al-Bashir awasili Ethiopia kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Afrika mashariki uliolenga kufungua njia kwa kura ya maoni ya Sudan kusini.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, aliwasili katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa Jumatatu jioni kwa mkutano wa viongozi wa Afrika mashariki uliolenga kufungua njia kwa kura ya maoni mwezi January mwaka ujao kwa ajili ya uhuru wa Sudan kusini.

Bwana Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC, kwa makosa ya uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki yanayohusu ukatili uliofanywa na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali huko magharibi mwa Sudan katika mkoa wa Darfur.

Ethiopia sio mwanachama wa ICC na hivyo haiwajibiki kumkamata Bashir. Mkutano huo ambao umefanywa chini ya udhamini wa IGAD, uliakhirishwa mwishoni mwa mwezi Oktoba kufuatia rais wa Sudan kupanga kuhudhuria.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba mkutano ulihamishiwa Ethiopia kutoka Kenya baada ya makundi ya kiraia nchini Kenya kupinga mpango wa bwana Bashir kuhudhuria na ICC kuitaka Kenya kumkamata bwana Bashir kama angeingia nchini humo.


XS
SM
MD
LG