Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 01:57
VOA Direct Packages

Baraza la waprotestanti la Rwanda kusitisha utoaji mimba kwenye vituo vyake vya afya kwa misingi ya kidini


Picha ya kanisa kutoka maktaba

Baraza la makanisa ya kiprotestanti nchini Rwanda limeamuru vituo vyake vyote afya nchini visitishe huduma za utoaji mimba, na kuifanya hali kuwa ngumu zaidi kwa wale wanaohitaji huduma hiyo kwenye taifa hilo la kikiristo lenye wakazi milioni 13. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mapema mwezi huu baraza hilo lilifanya uamuzi kuwa utoaji mimba kuwa ni dhambi, na kuunga mkono msimamo ambao unafuatiliwa sana na kanisa katoliki lakini kuna habari mkanganyiko na sheria za nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo inaruhusu utoaji mimba kwa sababu maalum.

Taarifa ilitiwa saini na taasisi za 26 za kiprotestanti badala ya kuwataka wazazi kutoa muongozo kwa binti zao kujizuia kufanya mapenzi mpaka atakapoolewa. Utoaji mimba ni kinyume cha sheria nchini Rwanda na pia adhabu ya kifungo kwa mtu yeyote ambaye alitoa mimba au alisaidia katika utoaji mimba.

Hata hiyo marekebisho ya sheria yalifanyika 2018 na kuruhusu utoaji mimba kutokana na mazingira kama vile ubakaji, ndoa za kulazimishwa, ngono kati ya wanafamilia, na pale ambapo mimba inahatarisha maisha ya mjamzito. Sheria hiyo inaruhusu utoaji mimba kupitia uamuzi wa daktari pekee.

Wakati akizungumza na shirika la habari la AP, mkuu wa kanisa la ki Anglikana nchini Rwanda Laurent Mbanda amesema kwamba wanazingatia imani yao ambayo haiwezi kuondolewa kwa kutumia sheria. Amesema kwamba hawapingi sheria, lakini Imani ni kinyume na utoaji mimba.

Amesema kuwa njia pekee kwa vituo vya afya vya baraza la kiprotestanti kukabiliana na suala hilo, ni kutuma wagonjwa kwenye hospitali nyinginezo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG