Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 03:55

Baraza la Usalama lajadili uharamia Pembe ya Afrika


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilianza kujadili utaratibu wa kukabiliana na uharamia kando ya pwani ya Somalia na namna ya kuwafungulia mashtaka na kuwahukumu maharamia.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeanza kujadili ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa Ban Ki-moon, ambayo inayotowa mapendekezo saba juu ya namna ya kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wa uharamia, katika siku za baadaye.

Mapendekezo hayo ni pamoja na kuimarisha mahakama za Somalia, hadi katika nchi nyengine za kanda hiyo na kuundwa kwa mahakama ya kimataifa kukabiliana na uharamia.

Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya mashambulizi ya uharamia nje ya mwambao wa Somalia ingali inaongezeka, lakini, mafanikio ya mashambulizi hayo yamepunguka, hiyo ikiwa ni kwa sababu ya kuongezwa kwa doria za majeshi ya majini kutoka nchi mbali mbali za dunian kwenye pembe ya Afrika na ghuba ya Aden.

Lakini tangu Mei 15 mwaka huu, mabaharia 450 wangali wanashikiliwa kwenye meli zilizotekwa na maharamia nje ya mwambao wa Somalia.

Bw. Ban aliliambia Baraza la Usalama la Umoja Mataifa, kuwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita, matukio 139 yanohusiana na uharamia, yalitokea nje ya pwani ya Somalia, na meli 30 zimetekwa nyara. Anasema Jumuiya ya Kimataifa imefanya juhudi katika miaka mitatu iliyopita kukabiliana na tatizo hilo, lakini akaongeza kuwa wanaweza kufanya zaidi.

"Kupunguza na kusitisha uharamia katika eneo hilo kutamaanisha kuendelea kufwatilia sio tu baharini lakini pia kwenye nchi kavu ambako uharamia unaanzia."

XS
SM
MD
LG