Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 21:49

Baraza la Usalama lawataka wakongo kuongoza utaratibu wa amani


wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa watembelea kambi ya Mugunga III camp Goma, wanakoishi watu walopoteza makazi yao mashariki ya DRC
Mabalozi 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waliondoka Goma jumapili jioni wakitoa wito kwa wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuchukuwa uwongozi na udhibiti wa utaratibu wa amani unaotokana na makubaliano ya Addis Abeba.

Akizungumza na waandishi habari kwenye uwanja wa ndege wa Goma mkuu wa ujumbe huo balozi wa Moroco kwenye Umoja wa Matiafa Mohammed Loulichki amesema "Baraza la Usalama limefika hapa ili kulihamasisha taifa la Kongo na mataifa ya kanda kuchukuwa udhibiti wa utaratibu wa amani. hii ni kwa sababu nyini ndio watu mtakaoleta amani, bila shaka pamoja na msaada wa MONUSCO."

Ujumbe huo wa Baraza la Usalama uliwasili Goma jumapili asubuhi kutoka Kinshasa ambako ulikutana na Rais Joseph Kabila na mawaziri wa serikali na kuelekea moja kwa moja hadi mlima Kibati ambako wapiganaji wa M23 walishindwa na majeshi ya serikali na Umoja wa Mataifa..

Katika mazungumzo yao na mawaziri wa ulinzi, sheria na wa mambo ya ndani wameitaka serikali ya Kinshasa kuwahukumu maafisa na wanajeshi wa jeshi la serikali walohusika na ubakaji wa wanawake na wasichana 130 katika mji wa Minova mashariki ya nchi.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power, amesema serikali inabidi kuonesha kwa vitendo kile inachohubiri kwa kuwaadhibu maafisa na wanajeshi walohusika. Anasema waliwaeleza bayana juu ya ukosefu wa maendeelo kuhusiana na suala hilo.

Mabalozi hao watatembelea Rwanda na Uganda ili kufuatilia jinisi utaratibu wa amani unavyoendelea kabla ya kwenda Addis Abeba kukutana na viongozi wa Ethopia na wanachama wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.
XS
SM
MD
LG