Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 26, 2023 Local time: 06:36

Baraza la usalama la UN litakutana kuhusu Jamhuri ya Watu wa Korea


Linda Thomas-Greenfield, Balozi wa Marekani katika UN

“Hiki ni kikao cha kwanza cha Baraza la Usalama cha wazi kuhusu hali ya haki za binadamu huko Korea Kaskazaini tangu mwaka 2017” amesema Balozi Thomas- Greenfield.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alitangaza Alhamisi kuwa Baraza la Usalama la Umoja huo litakutana kuhusu Jamhuri ya Watu wa Korea kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ukiukaji mwingine pamoja na uhusiano wake kwa amani na usalama wa kimataifa.

Balozi Greenfield alisema kikao hicho kitafanyika Agosti 17. Mkutano huo uliombwa na Marekani, Albania, Japan na Jamhuri ya Korea.

Akitangaza mkutano huo kwa wadhifa wake Thomas-Greenfield alisema mkutano huo tayari umechelewa mno. “Hiki ni kikao cha kwanza cha Baraza la Usalama cha wazi kuhusu hali ya haki za binadamu huko Korea Kaskazaini tangu mwaka 2017” amesema balozi Thomas- Greenfield.

Forum

XS
SM
MD
LG