Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura Ijumaa kuondoa vikwazo vya mwisho vya kupeleka silaha kwa serikali ya Somalia na vikosi vyake vya usalama, wanadiplomasia wamesema, zaidi ya miaka 30 baada ya vikwazo vya silaha kuwekwa kwa mara ya kwanza dhidi ya nchi hiyo.
Baraza hilo liliweka vikwazo dhidi ya Somalia mwaka 1992 ili kupunguza mtiririko wa silaha kwa wababe wa kivita, ambao walimuondoa madarakani dikteta, Mohamed Siad Barre na kuitumbukiza nchi hiyo ya Pembe ya Afrika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Baraza hilo lenye mataifa wanachama 15 linatarajiwa kupitisha maazimio mawili yaliyoandaliwa na Uingereza siku ya Ijumaa, wanadiplomasia wamesema, moja ya kuondoa vikwazo kamili vya silaha dhidi ya Somalia na nyingine ili kurejesha vikwazo vya silaha dhidi ya wanamgambo wa Al Shabaab wenye uhusiano na al-Qaeda.
Moja ya rasimu ya maazimio inasema kwamba “ili kuepuka wasi-wasi, kwamba hakuna vikwazo vya silaha kwa Serikali kuu ya Jamhuri ya Somalia."
Forum