Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:36

Baraza la mawaziri China kuhamasisha ufufuaji wa matumizi katika uchumi


Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang
Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang

Katika mkutano ulioongozwa na Waziri Mkuu Li Keqiang, baraza la serikali ya China ambalo linafanya kazi kama baraza la mawaziri liliapa kuharakisha utoaji wa miradi ya uwekezaji wa kigeni, kuendeleza uthabiti wa sarafu ya China ya Yuan, kurahisisha usafiri katika mipaka ndani na nje ya nchi

Baraza la mawaziri la China limesema Jumamosi kwamba litahamasisha ufufuaji wa matumizi kama kichocheo kikubwa cha uchumi na kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka nje, kituo cha televisheni cha taifa CCTV kimeripoti, wakati ambapo kuna upungufu wa mahitaji ya dunia huku mataifa makubwa kiuchumi yakielekea ukingoni mwa hali ya kudorora kwa uchumi.

Katika mkutano ulioongozwa na Waziri Mkuu Li Keqiang, baraza la serikali ya China ambalo linafanya kazi kama baraza la mawaziri pia liliapa kuharakisha utoaji wa miradi ya uwekezaji wa kigeni, kuendeleza uthabiti wa sarafu ya China ya Yuan, kurahisisha usafiri wa mipakani na kuyasaidia makampuni kushiriki katika maonyesho ya biashara ndani na nje ya nchi.

Baraza la mawaziri pia limethibitisha uungaji mkono wake kwa sekta binafsi na jukwaa la uchumi wa kidijitali, ambao umeondoa msururu wa kanuni zaz udhibiti katika miaka ya karibuni.

Pia ilijadili hatua za kuwasaidia wakulima kuanza upandaji wa kutumia chemchemi, ikiwa ni pamoja na ruzuku ya kupanda maharage ya soya, CCTV iliripoti.

Wakati wa likizo ya wiki nzima ya mwaka mpya wa kichina wa Lunar iliyomalizika Ijumaa, matumizi yaliongezeka kwa asilimia 12.2 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, mamlaka ya ushuru ilisema Jumamosi, ikionyesha kuongezeka tena baada ya kulegezwa kwa baadhi ya vizuizi vikali zaidi vya COVID-19 duniani.

XS
SM
MD
LG