Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:30

Baraza la mahakama laondolewa Hong Kong


Dazeni ya wanaharakati wanaoshtakiwa kwa uvunjifu wa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong kwa sasa watashitakiwa bila kuwepo kwa baraza la mahakama kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.

Jumla ya watu 46 wanakabiliwa na kesi baada ya kushtakiwa kwa kutotii sheria miezi 18 iliyopita na zaidi 30 wameshikiliwa bila ya kupewa dhamana.

Hatua za awali za kesi hizo zilianza mwezi Juni.

Waziri mpya wa mambo ya sheria wa Hong Kong, Paul Lam, aliamua kuondoa baraza la mahakama, akielezea wasiwasi wa usalama kwa wale wanaounda baraza la mahakama na familia zao.

Kwa kipindi cha miaka 177 kesi zimekuwa zikiendeshwa mbele ya baraza la mahakama na kutambuliwa katika mfumo wa kisheria.

Lakini toka Beijing kuweka sheria ya usalama wa taifa Hong Kong miaka mitatu iliyopita, kesi muhimu chini sheria ya usalama wa taifa zimekuwa zikiendeshwa na majaji maalumu waliochaguliwa.

XS
SM
MD
LG