Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:49

Bao la dakika za mwisho la kusawazisha larudisha matumaini ya Algeria  


Baghdad Bounedjah wa Algeria, kulia, akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili katika mchezo wa Kundi D wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Algeria na Burkina Faso Uwanja wa Peace of Bouake mjini Bouake, Ivory Coast, Jumamosi, Jan. 20, 2024. (AP).
Baghdad Bounedjah wa Algeria, kulia, akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili katika mchezo wa Kundi D wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Algeria na Burkina Faso Uwanja wa Peace of Bouake mjini Bouake, Ivory Coast, Jumamosi, Jan. 20, 2024. (AP).

Algeria walipata bao la kusawazisha katika  dakika za lala salama na kuepuka kufungwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumamosi  na kupata sare ya 2-2 na Burkina Faso katika Kundi D mjini Bouake.

Algeria walipata bao la kusawazisha katika dakika za lala salama na kuepuka kufungwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumamosi na kupata sare ya 2-2 na Burkina Faso katika Kundi D mjini Bouake jambo ambalo liliwaepusha mabingwa hao wa mwaka 2019 na kupata rekodi ya kushindwa katika michuano hiyo.

Mchezaji Baghdad Bounedjah alifunga mpira wa kona dakika tano ndani ya dakika ya lala salama na kuhakikisha timu yake ina wanyima Burkina Faso nafai ya waziya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata.

Bounedjah alifunga mabao yote ya Algeria huku Mohamed Konate na Bertrand Traore wakiifungia Burkinabe, ambao wanasalia kileleni mwa kundi D kwa pointi nne ikilinganishwa na mbili za Algeria.

Burkina Faso walikaribia kupata ushindi ambao ungewafanya kutinga hatua ya 16 bora wakiwa na uhakika wa kumaliza katika nafasi mbili za juu. Walikuwa chini ya shinikizo kwa muda mwingi wa mechi lakini maamuzi mawili ya VAR yaliwasaidia.

Forum

XS
SM
MD
LG