Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 09:49

Ban Ki Moon azitaka Sudan na Sudan Kusini kukutana haraka.


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ametoa onyo kwa Sudan na Sudan Kusini kukutana haraka kutokana na kitisho cha vita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon amezitaka Sudan na Sudan Kusini kukutana haraka iwezekanavyo kusuluhisha mvutano kati ya nchi hizo mbili lakini mkutano uliopangwa kufanyika Jumanne umevunjwa.

Marais wa nchi hizo wanatarajiwa kufanya mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. Wimbi la mashambulizi ya kijeshi lilipuka wiki iliyopita huku kila upande ukimlaumu mwenzake kwa kuanzisha mapigano.

Eric Reeves mtafiti wa Sudan na Sudan Kusini aliyepo Marekani aliiambia VOA kuwa kuhatarisha mkutano huo kunaweza kuwa kile ambacho baadhi ya maafisa wa juu wa jeshi wanalenga.

Amesema anafikiri nchi hizo mbili zinaweza kuwa karibu zinaenda vitani.

XS
SM
MD
LG