Upatikanaji viungo

Ban Ki Moon ataka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali dhidi ya Syria.

  • Sunday Shomari

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ataka baraza la usalama kuchukua hatua.

Nchi za magharibi zinaweka msukumo lakini Russia na China wamezuia hatua hizo.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon amelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali dhidi ya Syria ambapo anasema waathirika katika upinzani uliodumu kwa miezi 10 umefikia hatua ambayo haikubaliki.

Akiongea Jumatatu katika ziara huko Abu Dhabi Bw. Ban alitaka baraza la usalama kufanya kazi kwa uhakika katika kutafuta suluhu ya mzozo wa Syria.

Nchi zenye nguvu za magharibi zimekuwa zikiweka msukumo kwa miezi kadhaa kulaani ukandamizaji wa serikali ya Syria dhidi ya upinzani huo lakini Russia na China wamezuia hatua hizo.

XS
SM
MD
LG