Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:06

Ban aipongeza Liberia kwa kudumisha amani


Rais Barack Obama wa Marekani akihutubia mkutano mkuu wa UM mjini New York, 23 Sept. 2010
Rais Barack Obama wa Marekani akihutubia mkutano mkuu wa UM mjini New York, 23 Sept. 2010

Katibu mkuu wa Umoja wa Matiafa Ban Ki-moon anaipongeza Liberia kwa maendeleo ya kudumisha amani na kupambana na ulaji rushwa, alipokutana na rais Johnson Sirleaf kando ya mkutano mkuu unaoendelea huko New York.

Viongozi hao wawili walizungumza pia juu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu wa rais na bunge wa Liberia hapo mwakani, na mustakbal wa kikosi cha amani cha Umoja wa Mataifa nchini Liberia. Siku ya Jumatano Baraza la usalama la UM liliidhinisha kwa sautimoja kuongeza muda wa kikosi cha amani huko Liberia kwa mwaka mmoja zaidi.

Katika mkutano mkuu siku ya Jumamosi pia, rais wa Somalia Shiekh Sharif Shiekh Ahmed aliwambia viongozi wa dunia kwamba kuchelewa kuchukuliwa hatua kukabiliana na hatari iliyowazi kwa wakati huu kutanongeza hali ya ukosefu wa uthabiti katika Pembe ya Afrika na ugaidi wa kimataifa.

Aliihimiza Jumuia ya Kimataifa kukabiliana na vitisho vinavyosababishwa na kundi la kigaidi la Somaliala al-Shabab, lenye ushirikiano na al-Qaida.

Rais Sheikh Ahmed amelihimiza pia baraza la Usalama kupitisha azimio lenye lengo la kuepusha kuenea kwa magaidi wa al-Qaida na matawi yao katika nchi mbali mbali kama vile al-Shabab.

Siku ya Ijuma Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu mkuu Ban KI-moon wametoa wito kwa serikali za Sudan ya Kaskazini na Kusini kaunda kura ya maoni na lazima ufanyike kama ulivyopangwa mwezi Januari. Bw Ban vile vile ameteua jopo maalum la watu watatu litakaloongozwa na rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa kwenda kufuatilia matayarisho ya kura ya maoni.

Kwa upande wake rais wa visiwa vya Comoro Ahmed Abdallah Sambi aliionya Jumuia ya Kimataifa kwamba kukata kwa Ufaransa kutambua kwamba kisiwa cha Mayotte ni sehemu ya visiwa vya Comoro kutaweza kuweka dosari katika sifa na uwaminifu wa Umoja wa Matiafa.

Kwa muda wa wiki mbili kila mwaka Viongzi wa Dunia hukutana mjini New York Makao makuu ya Umoja wa mataifa kujadili masuala mbali mabli ya dunia na kueleza juu ya matakwa na mipango yao kwenye jukwa la kimataifa.

XS
SM
MD
LG