Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 23:07

Baltimore sasa ni shwari


Baadhi ya shughuli zimerejea katika hali ya kawaida leo katika mji wa mashariki mwa marekani wa Baltimore.

Shule zimefunguliwa ambapo wanafunzi walikwenda madarasani kama kawaida baada ya kuondoka kwa hali ya hofu.

Katika baadhi ya mitaa watu walionekana wakielekea makazini tofauti na siku ya Jumaane, kufuatia ghasia za Jumatatu.

Polisi wa mji huo wanasema kwamba kwa sasa mji upo shwari.

Ni watu kumi tu waliokamatwa mpaka sasa, katika usiku wa kwanza wa saa saba za amri ya kutotoka majumbani.

Polisi na vikosi vya ulinzi walipokabiliana na waandamanaji wachache hata wale baadhi waliokuwa wanawazomea na kuwarushia chupa za maji.

Ilikuwa tofauti kabisa na maandamano ya Jumatatu yaliyo ambatana na ghasia za uvunjifu wa sheria na wizi wa mali.

XS
SM
MD
LG