Mataifa ya Afrika mashariki Jumatano yamesoma mapendekezo ya bajeti zao kwa mwaka wa fedha kwa kipindi cha mwaka 2016/17, lakini nchini Uganda shughuli hiyo inasemekana kukumbwa na hali ya sintofahamu kutokana na kutokuwa na waziri wa fedha. Lakini Rais Museveni alimteuwa mbunge Mataiya Kasaija kuwasilisha hotuba hiyo ya bajeti.
Mwandishi wetu wa Kampala, Kennes Bwire anaeleza bajeti hiyo ni kubwa katika historia ya Uganda ikifikia shilingi trilioni 26 .
Wananchi wa Uganda inaripotiwa hawaoni afueni yeyote katika bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka huu.