Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:44

Bahrain yatangaza hali ya dharura


Wanajeshi wa Saudi Arabia wakielekea nchini Bahrain.
Wanajeshi wa Saudi Arabia wakielekea nchini Bahrain.

Bahrain imetangaza hali ya dharura kufuatia wiki kadhaa za ghasia. Televisheni ya taifa imetangaza jana kwamba majeshi ya usalama huenda yakachukua hatua muafaka kulinda taifa hilo kwa miezi mitatu ijayo.

Wanajeshi kutoka nchi jirani ya Saudi Arabia wamepelekwa Bahrain Jumatatu kulisaidia jeshi la nchi hiyo. Mataifa mengine ya ghuba pia yameahidi kutoa msaada.

Maendeleo hayo yamekuja baada ya waandamanaji kufunga barabara ambazo zinaelekea katikati ya mji mkuu siku ya jumapili na mapambano kusababisha watu zaidi ya 200 kujeruhiwa. Kusambaa kwa mapambano kumeriporiwa tena hivi leo Jumanne.

Serikali ya Bahrain inasema hatua zote muhimu lazima zichukuliwe ili kulinda usalama wa nchi, na kuongezea kwamba hali ya dharura imewekwa baada ya taasisi za Bahrain, uchumi na raia kutishiwa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Brookings huko Doha, Salman Shaikh anaamini kuwa mivutano huenda ikasambaa katika siku zijazo na kuongezea kuwa haya ni maendeleo yanayotia wasi wasi.

Waandamanaji wengi wao kutoka dhehebu la Shia huko Bahrain, walianza maandamano ya kudai haki zaidi na usawa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Baada ya ukamataji wa kutisha uliofanywa na utawala wa wasunni walio wachache, waandamanaji walianza kudai kuwepo kwa serikali mpya.

iran, taifa ambalo linatawaliwa na washia walio wengi nchini humo, limekosoa upelekaji wa wanajeshi wa kigeni huko Bahrain.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Ramin Mehmanparast amesema uingiliaji wa kigeni huenda usisuluhishe matatizo ya ufalme huo.

Bwana Mehmanparast amesema uingiliaji wa kigeni na ukandamizaji unaongezeka na mapambano ya ghasia si suluhisho kwa madai halali ya watu wa Bahrain.

Licha ya maoni hayo, wachambuzi wengi, kama Gala riani wa IHS global Insight hawaamini Iran ina nia ya dhati ya kuingilia kati hali ya huko.

XS
SM
MD
LG