Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:54

Bado imekuwa vigumu kupata Spika wa bunge la Marekani


Kundi la wabunge 20 wa mrengo wa kulia walimzuia tena Mbunge wa California Kevin McCarthy siku ya Alhamisi kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani.

Hoja kubwa ya wabunge hao ni misingi kwamba McCathy haonekani ni Mkonsevativ wa kutosha.

Siku ya tatu ya kupiga kura kumchagua kiongozi mpya wa baraza la kuu la bunge lenye wajumbe 435 ilikuwa kama siku mbili za kwanza, huku McCarthy, akipungukiwa na wingi wa kura 218 ambazo anahitaji kushinda.

Jumla ya Warepublikan 201 walimuunga mkono katika duru ya saba na nane ya upigaji kura, idadi sawa aliyokuwa nayo katika baadhi ya kura sita za awali siku ya Jumanne na Jumatano, ingawa alitoa maafikiano mapya juu ya sheria zinazosimamia shughuli za Bunge.

Katika awamu ya tisa ya upigaji kura, McCarthy alipata kura 200 kwa sababu Mwakilishi wa Republikan, Ken Buck hakuwepo alikuwa anahudhuria matibabu.

XS
SM
MD
LG