Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 21:01

Bachelet atoa wito kwa Rais Putin kusitisha  mashambulizi Ukraine

UN High Commissioner for Human Rights Michelle anahudhuria mkutano wake wa mwisho wa wanahabari kabla ya mwisho wa mamlaka yake katika Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi, Agosti 25, 2022. REUTERS/Pierre Albouy.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet siku ya  Alhamisi alitoa wito kwa Rais wa Russia Vladimir Putin kusitisha  mashambulizi ya silaha dhidi ya Ukraine.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet siku ya Alhamisi alitoa wito kwa Rais wa Russia Vladimir Putin kusitisha mashambulizi ya silaha dhidi ya Ukraine.

Akizungumza siku moja baada ya mzozo huo kufikia miezi sita, Bachelet aliangazia hali kuhusu kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, akisema mapigano katika eneo hilo yanaleta hatari isiyoweza kufikirika kwa raia na mazingira.

Russia and Ukraine wamelaumiana kwa mashambulizi karibu na kinu hicho na shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki limesema liko tayari kutuma wataalam wake katika eneo hilo kuhakikisha usalama wake.

Bachelet pia alisema Alhamisi kwamba vikosi vya Russia na Ukraine lazima viheshimu sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamu, wakati jumuiya ya kimataifa inapaswa kuhakikisha uwajibikaji kwa ukiukaji.

XS
SM
MD
LG