Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 15:59

Baba Mtakatifu Fransis kuwasili Marekani Jumanne


Baba mtakatifu Fransis akiwa Santiego

Francis alitembelea madhabahu hayo Jumatatu jioni baada ya kufika Santiago na kuongoza maombi mafupi ya kuwaunganisha watoto waliotawanyika kote duniani.

Mkuu wa kanisa katoliki baba Mtakatifu Francis anatazamikwa kuwasili Marekani Jumanne jioni baada ya kuongoza misa ya tatu na ya mwisho katika taifa la kikomunisti la Cuba.

Baba Mtakatifu anatarajiwa kukamilisha misa hiyo kwenye hekalu la bikira wa ukarimu wa El Cobre.

Francis alitembelea madhabahu hayo Jumatatu jioni baada ya kufika Santiago na kuongoza maombi mafupi ya kuwaunganisha watoto waliotawanyika kote duniani.

Babab Mtakatifu huyo mwenye umri wa miaka 78 alionekana mwenye maumivu wakati wa ziara hiyo labda kutokana na hali inayojulikana kama Sciatica inayosababisha maumivu kwenye mgongo na mguu.

Alikuwa amewasili kutoka mji wa Holguin ambako Jumatatu alihutubia maelfu ya waumini akiwahimiza kumfuata Yesu ili waepuke kupinga mabadiliko.

XS
SM
MD
LG