Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:52

Baba ya hayati mwanaharakati wa Iran aachiliwa huru


Waandamanaji wakiwa wameshika bendera walipokusanyika katika uwanja wa Trafalgar Square, jijini London, Jumamosi, Septemba 16, 2023 kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mahsa Amini nchini Iran. (Picha ya AP).
Waandamanaji wakiwa wameshika bendera walipokusanyika katika uwanja wa Trafalgar Square, jijini London, Jumamosi, Septemba 16, 2023 kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mahsa Amini nchini Iran. (Picha ya AP).

Baba yake Mahsa Amini alikamatwa kwa muda mfupi siku ya Jumamosi, mashirika ya kutetea haki za binadamu yalisema, huku kukiwa na uwepo mkubwa wa kikosi cha usalama kwenye kumbukumbu ya kifo cha binti yake katika kizuizi cha polisi cha Iran ambacho kilizua miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali.

Amjad Amini alionywa dhidi ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha bintiye kabla ya kuachiliwa huru mtandao wa Haki za Kibinadamu wa Kurdistan ulisema. Shirika rasmi la habari la IRNA la Iran lilikanusha kuwa Amjad Amini alikamatwa, lakini halikusema ikiwa alizuiliwa kwa muda mfupi au alionywa.

Hapo awali, mitandao ya kijamii na ripoti za mashirika ya kutetea haki za binadamu yalieleza kuhusu vikosi vya usalama kuchukua nyadhifa karibu na nyumba ya Amini huko Saqez, magharibi mwa Iran.

Kifo cha msichana huyo wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22 chini ya ulinzi wa polisi wa maadili mwaka jana kwa madai ya kukiuka kanuni za lazima za mavazi ya Jamhuri ya Kiislamu kilisababisha maandamano ya miezi kadhaa ambayo yalionyesha upinzani mkubwa zaidi kwa mamlaka katika miaka mingi iliyopita.

XS
SM
MD
LG