Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 15:11

Baadhi ya watu walioongoza mashambulizi kwenye bunge la Marekani wahukumiwa


Baadhi ya waandamanaji wa kundi la Proud Boys nje ya jengo la bunge. Jan 6, 2021
Baadhi ya waandamanaji wa kundi la Proud Boys nje ya jengo la bunge. Jan 6, 2021

Watu wawili waliokuwa viongozi wa kundi lenye msimamo mkali wa kulia la Proud Boys Alhamisi wamehukumiwa kifungo cha jela cha zaidi ya muongo mmoja kila mmoja, kutokana na kuongoza shambulizi kwenye majengo ya bunge la Marekani.

Watu hao wanatuhumiwa kuzuia ubadilishanaji wa amani wa madaraka kutoka kwa Donald Trump hadi kwa Joe Biden, baada ya uchaguzi wa rais wa 2020. Miaka 17 jela kwa kiongozi Joseph Biggs, na miaka 15 jela kwa mwenzake Zachary Rehi, ndivyo vifungo virefu zaidi kufikia sasa, dhidi ya watu walioshiriki kwenye shambulizi hilo la Januari 6, 2021.

Wawili hao ni wa kwanza kutoka kundi la Proud Boys kuhukumiwa na jaji wa Marekani Timothy Kelly ambaye pia atasikiliza kesi sawa na hizo za washukiwa wengine wawili ambao walipatikana kuwa na kesi ya kujibu hapo awali na jopo mwezi Mei.

Kusikilizwa kwa kesi yao kwa muda wa miezi minne hapa Washington kulifichua kwamba walikumbatia uongo wa Trump ambaye alikuwa mgombea wa Repablikan, kwamba uchaguzi uliibwa kutoka kwake.

Enrique Tarrio ambaye ni mkazi wa Miami na ambaye alikuwa mwenyekiti wa kitaifa wa Proud Boys amepangiwa kusomewa hukumu yake hapo Jumanne.

Forum

XS
SM
MD
LG