Hali hiyo imewalazimu kuitaka serikali kupitia upya baadhi ya sheria za kazi ambazo zinaonekana kuwapa mwanya wawekezaji wa kigeni kuendelea kuwakandamiza.
Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 kupitia kifungu cha 7 kukataza ubaguzi dhidi ya mfanyakazi katika sera ya ajira bado utekelezaji wake umegubikwa na vizingiti hasa pale inapo patikana taarifa ya kuvunjwa kwa sheria hiyo huku watanzania wakiwa wa athirika wakuu wa ubaguzi katika sehemu zao za kazi.
Kutokana na madai ya baadhi ya wafanyakazi dhidi ya ubaguzi kwenye maeneo yao ya kazi kuendelea kufanyika, imekuwa ni vigumu kutoa taarifa katika sehemu husika kwa kuhofia kupoteza ajira, suala linalo wafanya kuendelea kuumia na kuwaona wageni ambao wakati mwingine hawana fani yoyote kuneemeka kutokana na jitihada wanazo zifanya wao.
Wakati wafanyakazi wa viwandani wakiendelea kupitia ubaguzi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, ametaka kuorodheshewa majina ya viwanda vyote ambavyo vimekuwa sehemu ya malalamiko kwa Watanzania.
Amri Ramadhani Sauti ya Amerika Dar es Salaam
Facebook Forum