Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 03:28

Baadhi ya mataifa ya kiislamu yaitisha maandamano kupinga kuharibiwa kwa Quran nchini Sweden


Waandamanaji wakiruka uzio wa ubalozi wa Sweden mjini Baghdad, Alhamisi. Julai 20, 2023.
Waandamanaji wakiruka uzio wa ubalozi wa Sweden mjini Baghdad, Alhamisi. Julai 20, 2023.

Mataifa kadhaa ya kiislamu Ijumaa yameelezea kughadhabishwa na kuharibiwa kwa kitabu kitakatifu cha Quran nchini Sweden,wakati baadhi wakipanga kuandamana barabarani baada ya sala za Ijumaa.

Nchini Iran, Iraq na Lebanon, waandamanaji walijipanga baada ya polisi wa Sweden kuruhusu maandamano Alhamisi, ambapo raia mkristo kutoka Iran anayeishi Stockholm kurusha na kuharibu Quran, nje ya ubalozi wa Iraq nchini humo.

Saa kadhaa kabla ya tukio hilo, waandamanaji mjini Baghdad waliingia kwenye ubalozi wa Sweden na kuwasha moto ili kuonyesha ghadhabu yao kufuatia vitisho kutoka kwa mtu huyo kwamba angechoma Quran.

Waziri mkuu wa Iraq Shia al Sudani, ameamuru kufurushwa kwa balozi wa Sweden kutoka nchini humo pamoja na kuitwa nyumbani kwa mjumbe wa ubalozi wa Iraq aliyeko Sweden. Kando na hatua hizo, waandamanaji mjini Baghdad wamepanga kuendelea na maandamano hivi leo kueleza ghadhabu yao.

Forum

XS
SM
MD
LG