Waebrania weusi kama wanavyojulikana kwa kawaida hawajichukulii kuwa wayahudi, ingawa wanadai kuwa na historia ya taifa hilo. Kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiingia Israel, baadhi wakipewa haki za kuwa raia au vibali vya wakazi wa kudumu.
Hata hivyo 130 miongoni mwao hawana stakabadhi, na wameamrishwa kuondoka na serikali ya Israel. Takriban waebrania weusi 3,000 wanaishi kwenye miji iliyopo kusini mwa Israel, kitovu chao kikiwa mji wa Village of Peace ambao una majengo mafupi, na uliozungukwa na mimea na bustani.
Forum