Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 21:41

Baa la njaa lazidi kuuwa watu Somalia


Wakimbizi wa kisomali wakisubiri msaada wa chakula katika mji mkuu Mogadishu
Wakimbizi wa kisomali wakisubiri msaada wa chakula katika mji mkuu Mogadishu

Umoja wa Mataifa unakadiria watu milioni 11 katika eneo la pembe ya Afrika wanahitaji msaada wa dharura

Watu 10 wameripotiwa kufa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wakati majeshi ya Umoja wa Afrika na serikali yakipambana na wanamgambo kulinda chakula cha msaada.

Mashahidi walisema mapigano yalitokea wakati wa mapigano makali Alhamis, siku moja baada ya shirika la chakula Duniani-WFP, kudondosha tani 14 za chakula huko Mogadishu.

Watu 30 wameripotiwa kujeruhiwa wakati majeshi ya serikali na Umoja wa Afrika yalipopambana na wanamgambo wa kundi la al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaida ambalo limepiga marufuku msaada kutoka shirika la chakula la Umoja wa Mataifa.

Mashahidi wanasema majeshi yanayoiunga mkono serikali yameteka soko la Suq Ba’ad huko kati kati ya Mogadishu soko la pili kwa ukubwa katika mji mkuu.

Msemaji wa walinda amani wa Umoja wa Afrika, Luteni Kanali Paddy Ankunda anasema operesheni hiyo inalenga kuhakikisha kwamba mashirika ya kutoa msaada yanaweza kuendelea kufanya shughuli zao na kuwapa misaada muhimu inayohitajika wa-somali wanaotaabika na njaa.

Umoja wa Mataifa unaripoti kuwa wasomali 100,000 wamekimbilia Mogadishu hivi karibuni kutafuta maji na chakula ili kuokoa maisha yao.

Umoja wa Mataifa unakadiria watu milioni 11 katika eneo la pembe ya Afrika wanahitaji msaada wa dharura wakati eneo hilo linataabika na ukame mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miongo sita.

Umoja wa Mataifa umetangaza hali mbaya ya njaa katika maeneo mawili ya Sudan kusini yote ni ngome kuu ya kundi la al-Shabab.

Shirika la chakula Duniani-WFP linatarajia kudondosha vyakula zaidi kwa njia ya anga wiki hii kuelekea mashariki ya Ethiopia na kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka na Somalia.

Maelfu ya wasomali wanakatisha mpaka kuelekea kwenye makambi yaliyojaa wakimbizi nchini Kenya na Ethiopia.

XS
SM
MD
LG