Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 12, 2026 Local time: 02:58

Australia itashuhudia wanajeshi na vifaa zaidi vya kijeshi kutoka Marekani; Marles

Waziri wa ulinzi wa Australia Richard Marles(L) na Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa ulinzi wa Australia Richard Marles(L) na Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Marekani na Australia zilitangaza Jumamosi makubaliano ya kuongeza uwepo wa mzunguko wa vikosi vya Marekani na uwezo wake pamoja na kusaidia kuiunganisha Australia katika uwezo muhimu wa kuimarisha ulinzi wa Marekani kufuatia mazungumzo ya maafisa wa vyeo vya juu wa ulinzi wa Marekani na Australia.

Australia itashuhudia wanajeshi zaidi wa Marekani ikiwemo ndege, meli na silaha zaidi za Marekani wakati washirika hao wawili wakichukua kile maafisa wanakielezea kama hatua kubwa katika kuimarisha na kupanua ushirikiano wao wa kijeshi.

Marekani na Australia zilitangaza Jumamosi makubaliano ya kuongeza uwepo wa mzunguko wa vikosi vya Marekani na uwezo wake pamoja na kusaidia kuiunganisha Australia katika uwezo muhimu wa kuimarisha ulinzi wa Marekani kufuatia saa kadhaa za mazungumzo yaliyofanywa na maafisa wa vyeo vya juu wa ulinzi na kidiplomasia wa Marekani na Australia.

Australia kwa wakati huu haina rafiki bora kama Marekani, alisema waziri wa ulinzi wa Australia, Richard Marles akiwaambia waandishi wa habari kufuatia kukamilika kwa mashauriano ya 33 ya kila mwaka ya ngazi ya mawaziri ya Australia na Marekani mjini Brisbane nchini Australia.

Marles alisema makubaliano hayo yanajumuisha uwepo mzunguko mkubwa wa Marekani kwenye vituo vya jeshi la kaskazini mwa Australia ziara za ziada zinazofanywa na meli za marekani na doria za baharini pamoja na ndege za kubeba mizigo, na kuongezeka kwa safari za ziada kutoka kwenye manowari za nyuklia za Marekani, hadi Australia ipate uwezo wa kujiendesha yenyewe kwa msaada wa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG