Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 03:20

AU yatoa wito wa msaada kwa Comoros


Kituo kikuu cha kusafisha maaji cha Vouvuni kimeharibika kutokana na mafuriko.
Kituo kikuu cha kusafisha maaji cha Vouvuni kimeharibika kutokana na mafuriko.

Mafuriko kutokana na mvua za zaidi ya wiki moja yasababisha maafa na uharibifu mkuwa wa mali.

Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Jean Ping ametoa wito kwa mataifa ya Afrika na jumuia ya kimataifa kutoa msaada wa dharura kuisaidia Comoros kukabliana na maafa na hasara zinazotokana na mafuriko ya zaidi ya wiki moja.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, Bw. Ping alisema hali mbaya ya hewa imesababisha vifo vya watu na mali nyingi kuharibika, na akawahakikishia wananchi wa Comoros uungaji mkono wa AU.

Huko mjini Moroni, serikali ilitangaza rasmi kamati maalum ya kushughulikia kazi za dharura kutokana na mafuriko hayo ikieleza kwamba zaidi ya watu elfu 46 wameathirika, na watu elfu 9 kupoteza makazi yao.

Mohamed Mchangama mwanachama wa kamati hiyo ameiambia Sauti ya Amerika kwamba wananaza kazi ya kutathmini hasara zilizopatikana na kuwasaidia waathiriwa.

Anasema kiasi ya watu elfu 80 hawana maji katika mji mkuu wa Moroni na miji ya karibu, na waataalamu wanahofia kuzuka kwa kipindupindu na magonjwa yanayotokana na maji machafu.

XS
SM
MD
LG