Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:56

AU yasema kuna maendeleo katika mapambano dhidi ya LRA


Mwanajeshi wa Uganda akipambana na kundi la LRA kwenye mpaka unaopakana na CAR, Sudan Kusini na DRC.
Mwanajeshi wa Uganda akipambana na kundi la LRA kwenye mpaka unaopakana na CAR, Sudan Kusini na DRC.

Eneo la Umoja wa Afrika linalopambana na kundi la Lord’s Resistance Army linaripoti maendeleo katika jitihada za kulizorotesha kundi hilo la ugaidi. Lakini bila ya rasilimali zaidi kikosi cha eneo hilo huwenda kikahitaji miaka mingi zaidi kabla ya Joseph Kony na waasi wake kusambaratishwa na jeshi lake la watoto waliotoroshwa kuachiwa huru.

Kundi la Lord’s Resistance Army-LRA liliwahi kufahamika sana kwa kuchoma vijiji, kuwateka watoto na kuwakosesha makazi maelfu ya watu wakati wakilenga kuiangusha serikali ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Lakini anasema Luteni Jenerali Samuel Karuma, kundi hilo la msituni sasa limedhoofika baada ya kuundwa kwa kikosi maalumu kwenye eneo hilo na Umoja wa Afrika ikijumuisha wanajeshi kutoka Uganda, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC na Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR. “Tumepunguza nguvu zao kwa kuwauwa baadhi yao na kuwakamata baadhi yao. Kufikia kiwango cha kuwauwa viongozi wawili kwenye uongozi wao na makamanda wengine wengi wa cheo cha juu na baadhi ya makamanda wa vyeo vya juu pia wameasi”.

Waasi wa Lord's Resistance Army
Waasi wa Lord's Resistance Army

Kikosi hicho maalumu kina vituo kadhaa katika nchi zote nne zilizoathiriwa na LRA. Baada ya kundi hilo kufukuzwa nchini Uganda lilianza kuendesha harakati zake nchini Sudan Kusini. Inaaminika kuwa LRA hivi sasa limegawanyika katika makundi makubwa matano, mengi yanaendesha shughuli katika Jamhuri ya Afrika ya kati na katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Nchi hizi wanazitumia kujificha na kwa ajili ya rasilimali zao.

Nchi hizo nne ziliahidi jumla ya wanajeshi 5,000 ambapo 2,000 kutoka Uganda na 1,000 kutoka kila nchi tatu zilizosalia. Lakini kanali Mike Kabagno, kamanda wa kikosi cha Uganda katika CAR anasema hakuna nchi yeyote ambayo imeweza kupeleka idadi ya wanajeshi iliyoahidi.

“Hivi tunavyozungumza Uganda ina wanajeshi 1,500, tulikuwa 2,000 lakini kutokana na majukumu mengine tunaendelea kupungua na kuongezeka, Afrika ya kati wakati Bozize alipoondolewa madarakani kila mmoja alifedheheshwa. DRC wanajeshi 100 hadi 500 inaendelea kuongezeka na kushuka. Sudan Kusini hivyo hivyo wana matatizo ambapo idadi hivi sasa ni wanajeshi 100 hadi 200”.

Ghasia za kisiasa, migogoro na ukosefu wa rasilimali ulizuia nchi hizo kupeleka wanajeshi wanaohitajika ili kupambana na kundi la LRA.

Msaada wa anga unatolewa na Marekani, na Africom – kikosi cha Marekani katika Afrika pia wanatoa mafunzo. Lakini jeshi la Marekani halihusiki katika operesheni hizi.

XS
SM
MD
LG