Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 04:02

AU yasema ina wasiwasi mkubwa na kuzorota kwa usalama mashariki mwa Congo


Wakuu wa nchi za Afrika walipohudhuria Kikao cha 35 cha Bunge la Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia Jumamosi, Februari 5, 2022.
Wakuu wa nchi za Afrika walipohudhuria Kikao cha 35 cha Bunge la Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia Jumamosi, Februari 5, 2022.

Umoja wa Afrika siku ya Jumapili ulisema kuwa una wasiwasi mkubwa na kuzorota kwa hali ya usalama katika eneo lenye matatizo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako waasi wamepata mafanikio mapya.

Katika taarifa ya pamoja, mwenyekiti wa AU Macky Sall na mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat walisema "wanaelezea wasiwasi wao mkubwa" kutokana na kuzorota kwa usalama na wakaomba utulivu na mazungumzo.

Wanatoa wito kwa pande zote kuanzisha usitishaji vita mara moja, kuheshimu sheria za kimataifa, na usalama wa raia,” ilisema taarifa hiyo.

Waasi wa M23 waliteka maeneo zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yenye utajiri mkubwa wa madini siku ya Jumamosi, na kusababisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kuongeza "kiwango cha tahadhari" na kuongeza uungaji mkono kwa jeshi.

Hatua hiyo ya hivi punde ilikuja wakati uhusiano wa kidiplomasia kati ya majirani hao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda ikizidi kuwa mbaya kutokana na kuwaunga mkono waasi.

Mamlaka mjini Kinshasa, ambayo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, Jumamosi ilitangaza kuwa balozi wa Rwanda atafukuzwa, hatua ambayo Kigali ilisema inasikitisha.

AU ilizitaka pande zote kushiriki "katika mazungumzo ya kujenga" ili kuhakikisha amani katika eneo hilo lenye matatizo.

XS
SM
MD
LG