Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 08:55

AU kuzungumzia kesi za ICC zinazowahusu viongozi wa Kenya


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (L) na Naibu rais wake William Ruto wote wanashtakiwa na ICC huko The Haque
Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kufanya mkutano maalum mwezi ujao Addis Ababa, Ethiopia huku upinzani ukiongezeka kuhusu kesi za uhalifu dhidi ya ubinadamu zinazoukabili uongozi wa Kenya kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC.

Umoja wa Afrika-AU inaishutumu ICC yenye makao yake The Hague kwa kuwashitaki wa-Afrika na awali iliitaka mahakama hiyo kufuta kesi za Kenya. Maafisa wanasema AU hivi sasa inataka kesi zinazowahusu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto kuhamishiwa nchini Kenya.

Japokuwa wanadiplomasia wanasema hilo halionekani kwa nchi zote 34 wanachama wa AU ambao ni wanachama wa ICC kwamba watakuwa na mtizamo wa pamoja wa kujitoa katika taasisi hiyo, maafisa wanasema suala hilo litakuwa ajenda ya majadiliano.

Kenyatta na Ruto pamoja na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang wanakabiliwa na mashtaka dhidi ya uhalifu wa kibinadamu wakidaiwa kuhusika katika kupanga ghasia za kikabila baada ya uchaguzi mkuu uliokuwa na utata mwaka 2007 nchini Kenya. Ghasia kati ya jamii za makabila ya Kikuyu na Kalenjin zilisababisha vifo vya watu wasiopungua 1,100 na zaidi ya watu 600,000 walikoseshwa makazi.

Kesi ya Ruto na Sang tayari imeanza mwezi huu na kesi ya Rais Kenyatta imepangwa kuanza mwezi Novemba. Watatu hao kwa jumla wanashirikiana vizuri na mahakama hiyo ya ICC na wamekana mashtaka dhidi yao.
XS
SM
MD
LG