Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 09:39

Athari ya uharamia kwenye mwambao wa Afrika Mashariki


A handout picture received from The Netherlands Ministry of Defence shows a boat containing alleged Somali pirates being apprehended by Netherlands warship Evertsen acting as part of EU counter piracy operations at sea some 150 nautical miles off the coas

Utekaji nyara meli katika bahari ya Hindi umekuwa biashara kubwa kwa upande moja, lakini hasara kwa biashara ya wakazi wa Afrika Mashariki.

Mwezi Novemba mwaka 2011 kundi la kina mama liliwasili mbele ya ofisi za radio shirika ya Sauti ya Amerika, Baraka FM mjini Mombasa, Kenya, kudai hatua za serikali kuokoa waume zao ambao walikuwa wakishikiliwa mateka katika meli mbali mbali zilizotekwa na maharamia wa kisomali katika mwambao wa afrika mashariki.

Miongoni mwao alikuwa Mildred Otieno ambaye mume wake na shemegi yake walikuwa wanashikiliwa mateka kwa miezi kadha katika meli ya uvuvi ya Golden Wave baharini, huku yeye akiwa ameachwa nyumbani na watoto wawili bila msaada ya mume wake.

Mkasa wa Otieno na familia yake ni kielelezo cha athari za uharamia ambao umekuwa ukitokea katika mwambao mzima wa Afrika mashariki kwa kiasi cha miaka sita sasa. Maharamia wa kisomalia wamekuwa wakiteka nyara meli za mizigo, za uvuvi na hata meli za safari za starehe na kudai fidia ya mamilioni ya dola.

Idadi kamili ya meli ambazo zimekwishatekwa katika mwambao wa Afrika Mashariki ni vigumu kufahamiki kwa hakika, lakini kwa hivi sasa takwimu zinaonyesha kuna jumla ya meli 30 ambazo ziko mikononi mwa maharamia, na ndani yake mkiwa na wafanyakazi wapatao 800, wengi wao raia wa Afrika Mashariki.

Tangu mwaka 2005 mashirika mengi ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Shirika la Chakula Duniani, WFP yamekuwa yakilalamika kuhusu kuongezeka kwa gharama za usafiri baharini kutokana na uharamia. Karibu asilimia 90 ya shehena za misaada ya WFP inasafirishwa kwa njia za baharani, na sasa meli za mizigo ya misaada zinalazimika kusindikizwa na ulinzi wa kijeshi.

Andrew mwangura ni mwenyekiti wa chama cha mabaharia, Kenya. Kadhia ya utekaji nyara meli imekuwa moja ya sehemu kubwa ya kazi zake za kila siku tangu utekaji uanze kuibuka kwa wingi mwaka 2005.

Anaelezea ambavyo biashara ya usafirishaji ilivyoathirika na pia kuongeza gharama za bidhaa kwa wanunuzi nchi kavu.

Pengine hakuna biashara ambayo imeathirika vibaya zaidi na utekaji nyara wa meli kuliko biashara ya usafirishaji bidhaa katika Bahari Hindi. Kampuni za usafirishaji, kuanzia Zanzibar, Mombasa mpaka Somalia kwenyewe na kwa mapana zaidi hadi katika visiwa vya Comoro zimeona biashara zao zikipungua kwa kiasi kikubwa, na kusababisha hasara ya mamilioni ya dolla.

Baadhi ya kampuni katika miji ya Mombasa, Zanzibar, visiwani Comoro na Madagascar zimesimamisha kabisa shughuli zake kutokana na hofu ya maharamia katika mwambao wa afrika mashariki.

Karim Kudrat ni mfanya biashara wa usafirishaji baharini anayemiliki kampuni ya Motaku shipping mjini Mombasa, Kenya

Kwa vizazi kadha kazi ya ubaharia kwa wenyeji wa mwambao ya afrika mashariki imekuwa shughuli kubwa – iwe kazi katika meli za mizigo au meli kubwa za uvuvi.

Lakini katika kipindi cha miaka sita iliyopita mabaharia wamekuwa wakifanya kazi hiyo huku wakiwa na hofu ya kutekwa na maharamia. Wengi walishikwa mateka kwa miezi kadha na kutumiwa kama maharamia kuteka meli nyingine. John francis sanzige – ni mfanyabiashara wa kitanzania ambaye pamoja na mabaharia wa ms zulfikar yenye makao yake visiwani Comoro walitekwa na maharamiwa wa kisomali na kuzurura baharini kwa miezi kadha. Alizungumza na waandishi mwezi uliopita baada ya kuokolewa katika pwani ya madasgacar na kurejeshwa dare s salaam.

Umoja wa Ulaya ukishirikiana na Marekani umekuwa ukifanya doria katika pwani ya Afrika Mashariki, hali ambayo imepunguza utekaji nyara karibu na pwani. Hata hivyo, utekaji sasa umehamia katika bahari ya maji makuu ili kukwepa doria hizo. Marekani hivi sasa inashirikiana na serikali za Afrika Mashariki kutoa mafunzo ya ulinzi ili kupambana na uharamia katika mwambao wa afrika mashariki.

XS
SM
MD
LG