Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 07, 2024 Local time: 01:13

Assange kukiri mashitaka yake


Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange, atakiri mashtaka ya uhalifu katika makubaliano na wizara ya sheria Marekani ambayo yatasababisha kuachiliwa kwake kutoka gerezani.

Hatua hiyo itasuluhisha sakata la muda mrefu la kisheria ambalo limehusisha mabara mengi na lililojikita katika uchapishaji wa taarifa za siri, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizowasilishwa Jumatatu jioni.

Assange amepangiwa kufika katika mahakama ya serikali kuu ya Marekani katika visiwa vya Mariana, himaya ya Marekani katika Pasifiki Magharibi, kujibu mashtaka ya ujasusi wa njama za kupata na kusambaza habari za ulinzi wa kitaifa kinyume cha sheria, Wizara ya Sheria ya Marekani imesema katika barua iliyowasilishwa mahakamani.

Maombi ya kukubali mashitaka ambayo lazima yaidhinishwe na hakimu, yanahitimisha kesi ya jinai ya kimataifa na serikali ya Marekani kumfuatilia kwa muda mrefu mchapishaji ambaye tovuti yake maarufu ya taarifa za siri imemfanya kuwa maarufu kwenye vyombo vingi vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG