Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:33

Asplundh yatozwa faini kwa kuajiri wahamiaji haramu Marekani


Mfanyakazi mmojawapo katika kampuni ya Asplundh Tree.
Mfanyakazi mmojawapo katika kampuni ya Asplundh Tree.

Serikali ya Marekani imeitoza faini ya dola milioni 95 kampuni moja ya Marekani ya kukata miti kwa kuwaajiri wahamiaji haramu wakati ambapo ilifahamu kuwa ni kinyume cha sheria.

Waendesha mashtaka wanasema faini dhidi ya kampuni ya Asplundh Tree huko Philadelphia ni kiwango kikubwa kuwahi kutozwa katika kesi inayohusu uhamiaji.

Waendesha mashtaka wanasema mameneja wa kampuni hiyo kwa makusudi walipuuzia sheria wakati wasimamizi walipowaajiri wafanyakazi ambao ni wahamiaji haramu kati ya mwaka 2010 na 2014.

Hata hivyo waendesha mashtaka wanasema mwenendo huo uliifanya kampuni hiyo kuwa na nguvu kazi kubwa wakati wa dharura za hali ya hewa kote nchini na kuwaweka washindani wao katika nafasi isiyo nzuri kiushindani.

Uchunguzi wa serikali kuu kwa kampuni ya Asplundh Tree ulifunguliwa mwaka 2015 na kampuni imesema tangu wakati huo imechukua hatua kadhaa kufuta utaratibu wa zamani.

XS
SM
MD
LG