Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 04:18

Waziri wa ulinzi wa Marekani ahudhuria mkutano wa ulinzi Singapore


Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter
Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ash Carter, yuko nchini Singapore kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa usalama, ambao unaojumuisha mawaziri wa ulinzi na wakuu wa kijeshi kutoka ulimwenguni kote.

Carter yuko kwenye kongamano hilo la siku tatu ambalo linafahamika kama 'Shangri-la Dialogue', na anatarajiwa kutoa hotuba yake kesho Jumamosi.

Mazungumzo katika kikao hicho kitakachoendelea hadi siku ya Jumapili, huenda yakaangazia zaidi swala la China kuendelea kuongezeka kwa uwepo wake na ujenzi katika bahari ya China Kusini.

Carter alionya wiki jana kwamba China iko kwa hatari ya kujenga ukuta wa kujitenga kwa kuendelea na operesheni zake kwenye bahari ya China Kusini.

Nchi hiyo inadai umiliki wa bahari ya China Kusini, na imeendelea na ujenzi wa kambi ndogo kwenye visiwa vidogo katika bahari hiyo. Eneo hilo pia linadiawa na Ufilipino na Vietnam.

Kwa ujumla, serikali sita zinadai umiliki wa sehemu za eneo hilo, lenye utajiri wa raslimali.

XS
SM
MD
LG