Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:31

Rais wa Zambia awataka viongozi wa umma kutangaza mali zao


Rais mpya wa Zambia Michael Sata
Rais mpya wa Zambia Michael Sata

Rais mpya wa Zambia awataka viongozi wa umma kutangaza mali zao hadharani na aahidi kupambana na rushwa na umasikini.

Rais wa Zambia Michael Sata amerudia wito wake wa kupambana na rushwa. Akizungumza bungeni Ijumaa rais huyo mpya aliahidi kuchukua hatua za kupambana na rushwa wa kuwataka viongozi wa umma kutangaza mali zao hadharani.

Bw. Sata aliahidi pia kuchunguza tuhuma za rushwa za uongozi uliopita. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 alipata ushindi mkubwa dhidi ya kiongozi wa zamani Rupiah Banda katika uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita, akiwaambia wapiga kura kuwa atawasaidia masikini wan chi hiyo na kupambana na rushwa.

Awali mwezi huu Bw.Sata alimbadilisha Afisa wa juu wa kupambana na rushwa katika mlolongo wa hatua za kuisafisha serikali yake kutokuwa na mahusiano yeyote na mtangulizi wake.

Bw.Sata amerudia mara kadhaa shutuma kwamba Bw.Banda kwa kuvumilia rushwa na hakufanya vya kutosha kuhakikisha raia wengi zaidi wa Zambia wanapata kiasi cha utajiri wa shaba wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG