Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:51

Clinton azungumza na maafisa wa Misri


Rais wa Misri Mohammed Morsi
Rais wa Misri Mohammed Morsi

Waziri Hillary Clinton azungumza na Mohammed Tantawi

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amekutana leo mjini Cairo na mwanajeshi wa ngazi ya juu wa Misri Mohammed Hussein Tantawi siku moja baada ya kufanya mazungumzo na rais mpya nchini humo Mohammed Morsi. Clinton alisema Field Marshal Tantawi ambaye alikuwa kaimu kiongozi baada ya kutimuliwa madarakani kwa rais Hosni Mubarak, alijadilia maswala pana likiwemo swala la mchakato wa kisiasa, umuhimu wa kulinda haki za Wamisri wote na uthabiti wa kikanda. Clinton pia amezungumza na viongozi makundi ya kina mama na wale wa dini ya Kikristo kabla ya kuelekea mji wa Alexandria kwa sherehe za kupeperusha bendera ya Marekani katika ofisi ya kibalozi mjini humo. Ataondoka Misri baaadye Jumapili kuelekea Israel.

XS
SM
MD
LG