Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:55

Armenia yashutumu kundi la usalama la Russia kwa kushindwa kutoa ulinzi


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) katika kikao na waziri wa mambo ya nje wa Azerbaijan Jeyhun Bayramov na mwenzake wa Armenia Ararat Mirzoyan Nov 7,2022
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) katika kikao na waziri wa mambo ya nje wa Azerbaijan Jeyhun Bayramov na mwenzake wa Armenia Ararat Mirzoyan Nov 7,2022

Waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan Jumatano amelishutumu kundi la usalama linaloongozwa na Moscow kwa kushindwa kutoa ulinzi kwa nchi yake dhidi ya uvamizi wa adui yake mkubwa Azerbaijan.

Taarifa kutoka makao makuu ya nchi hiyo Yerevan imeishutumu Azerbaijan kwa kuikalia kimabavu sehemu yake ardhi yake kufuatia mapigano makali kati ya nchi hizo jirani yaliyotokea mwezi Septemba. Katika mapigano hayo watu zaidi ya 280 walipoteza maisha.

Armenia ni mwanachama wa Taasisi ya Umoja wa Nchi zilizosaini Mkataba wa uUalama, ukiongozwa na Moscow na jamhuri ya zamani za Umoja wa Sovieti.

“Mpaka sasa tumeshindwa kufanya maamuzi kuhusu majibu ya CSTO juu ya uvamizi wa Azerbaijan dhidi ya Armenia” Pashinyan alisema hayo Jumatano wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa umoja huo, akiwemo rais wa Russia Vladimir Putin uliofanyika huko Yerevan.

Amesema ilikuwa “huzuni kuona kuwa uanachama wa Armenia katika CSTO umeshindwa kudhibiti uvamizi wa Azerbaijani”

“Ukweli huu utaharibu kwa kiasi kikubwa sana sura CSTO kote ndani ya nchi yetu na nje “

Mwezi wa Septemba Armenia iliomba msaada wa kijeshi kutoka Moscow, ambayo kwa mujibu wa mkataba ilikuwa na wajibu wa kutoa ulinzi kwa Armenia pale inapokabiliwa na uvamizi wa nje.

Kremlin ambayo ina uhusiano wa karibu na Baku imeshindwa kutoa msaada wa haraka kwa Yerevan.

Pushnyan na Putin wanatarajiwa kukutana kwa mazungumzo zaidi.

Miaka ya 1990 na 2020 Armenia na Azerbaijan zilipigana vita mara mbili, kuhusu mgogoro wa eneo la Nagorno – Karabakh unaokaliwa na raia wa Azerbaijan wenye asili Armenian.

Wiki sita za mapigano katika kipindi cha vuli cha 2020 wanajeshi zaidi ya 6,500 kutoka pande zote mbili walipoteza maisha. Mapigano hayo yalisimama baada ya Russia kuingilia kati na kusimamisha mapigano.

Katika makubaliano Armenia ilipoteza eneo lake ambalo walilidhibiti kwa miongo kadhaa na Moscow ilipeleka kias cha walinzi wa amani wa Russia 2,000 kusimamia sitisho tete la mapigano.

Watu wenye asili ya Armenia wanalikalia Nagorno – Karabakh walijitenga kutoka Azerbaijan wakati Umoja wa Sovieti uliposambaratika mwaka 1991. Mgogoro katika eneo hilo ulisababisha vifo vya watu takribani 30,000.

XS
SM
MD
LG