Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:28

Ariel Castro afikishwa mahakamani Ohio


Ariel Castro aliyeteka nyara wasichana watatu kwa miaka 10, Cleveland, Ohio May 9, 2013
Ariel Castro aliyeteka nyara wasichana watatu kwa miaka 10, Cleveland, Ohio May 9, 2013

Kesi ya utekaji nyara wa wasichana watatu Marekani yashtua wengi Marekani na nje ya Marekani.

Dereva wa zamani wa basi la shule kutoka jimbo la Ohio, Marekani Ariel Castro anayeshutumiwa kuwashikilia mateka wanawake watatu katika nyumba yake kwa mwongo mmoja, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Alhamisi akiwa ameinamisha kichwa chake chini wakati jaji akiwa ameweka dhamana kubwa katika kesi yake. Castro hakusema lolote wakati wa kusomewa mashataka.

Jaji wa Cleveland katika jimbo la Ohio aliamuru kuachiwa kwake kwa dhamana ya dola milioni nane , kiasi ambacho Castro ambaye hana ajira hawezi kumudu na hivyo kubaki jela mpaka kesi yake itakaposikilizwa tena.

Mwendesha mashtaka alisema Castro aliwanyanyasa kingono wanawake aliowateka kati ya mwaka 2002 hadi 2004 na kuwaweka katika nyumba yake kwa mwongo mmoja. Mwendesha mashtaka alieleza kuwa wanawake hao hawakuruhusiwa kutoka ndani ya nyumba. Castro anakabiliwa na mashtaka matatu ya utekaji nyara na ubakaji wa Amanda Berry, Gina De Jesus na Michelle Knight.
XS
SM
MD
LG