Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:34

Trump apata uteuzi rasmi wa chama cha Republican kuwania urais


Mgombea urais wa Republican, Donald Trump.
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump.

Bila ya kutarajiwa akiwa ameingia katika nafasi ya juu kwenye uwanja wa siasa za Marekani, bilionea Donald Trump amepata rasmi uteuzi wa chama cha Republican kuwania urais kwa mujibu wa hesabu ya wajumbe iliyofanywa na shirika la habari la Associated Press-AP.

Akiwa amebakiwa na wagombea wachache kati ya 17 wa chama Republican waliokuwa wakiwania pamoja naye na hivyo kujiondoa mapema mwezi huu katika kinyang’anyiro AP imesema Trump ambaye aliwahi kuendesha kipindi cha televisheni hivi sasa anahakikishiwa kuwa ana wingi wa wajumbe 1,237 wanaohitaji katika mkutano mkuu wa Republican utakaofanyika mwezi Julai ambapo atateuliwa rasmi kuwania urais.

Donald Trump akiwa North dakota na wafuasi wake
Donald Trump akiwa North dakota na wafuasi wake

Anatarajiwa huenda akapata mamia ya wajumbe katika uchaguzi wa awali ambao utafanyika June 7. Nina heshima kubwa Trump aliwaambia waandishi wa habari katika jimbo la kaskazini la North Dakota na kuapa kwamba siku za kwanza za urais wake atatengua amri nyingi za kiutendaji ambazo zilitiwa saini na Rais Barack Obama na kulijenga tena jeshi la nchi.

XS
SM
MD
LG