Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 02:31

Antony Blinken yupo Saudi Arabia kwa mazungumzo na Mohammed bin Salman


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken (L) akiwa na mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken (L) akiwa na mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.

Wakati wa mkutano wao huko Jeddah, Blinken ameishukuru Saudi Arabia kwa msaada wake wa kuwahamisha raia wa Marekani kutoka Sudan na kwa kuandaa mkutano wa Muungano wa kuishinda ISIS. Pia walijadili kuhusu Yemen na kutafuta suluhisho la kisiasa ili kufikia amani huko, miongoni mwa masuala mengine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini Saudi Arabia Jumanne na kukutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Wakati wa mkutano wao huko Jeddah, Blinken ameishukuru Saudi Arabia kwa msaada wake wa kuwahamisha raia wa Marekani kutoka Sudan na kwa kuandaa mkutano wa Muungano wa kuishinda ISIS. Pia walijadili kuhusu Yemen na kutafuta suluhisho la kisiasa ili kufikia amani huko, miongoni mwa masuala mengine.

Waziri huyo wa mambo ya nje alisema kwamba uhusiano kati ya nchi zao mbili unaimarishwa na maendeleo ya haki za binadamu, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller alisema katika taarifa ya mkutano huo kati ya Blinken na mwana mfalme.

Blinken na mwanamfalme walijadili pia juu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, hasa katika nyanja za nishati safi na teknolojia. Kabla ya ziara hiyo, Blinken alisema Jumatatu kuwa Marekani ina maslahi ya kweli ya usalama wa kitaifa katika kukuza hali ya kawaida kati ya Israeli na Saudi Arabia.

Forum

XS
SM
MD
LG