Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 07:06

Anthony Albanese kiongozi wa chama cha Labor ashinda uchaguzi Australia


Anthony Albanese. kiongozi wa chama cha Labor na rafiki yake Jodie Haydon na mtoto wake Nathan Albanese akisherekea ushindi baada ya waziri mkuu Scott Morrison kukubali kushindwa huko Sydney Australia Mei 21,2022.(REUTERS/Jaimi Joy

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison alikubali kushindwa  siku ya Jumamosi na chama cha upinzani cha Labour  ambacho kilitazamiwa kumaliza takriban muongo mmoja wa utawala wa waconservative kwa uwezekano wa kuungwa mkono na watu huru wanaounga mkono mazingira.

Baadhi ya matokeo yalionyesha muungano wa Liberal National wa Morrison uliadhibiwa na wapiga kura katika eneo la Australia Magharibi na viti vya mijini kwa matajiri.

Usiku wa leo, nimezungumza na Kiongozi wa Upinzani na Waziri Mkuu ajaye, Anthony Albanese. Na nimempongeza kwa ushindi wake wa uchaguzi jioni hii," Morrison alisema, akijiuzulu kama kiongozi wa chama chake.

Labour walikuwa bado hawajafikia viti 76 kati ya 151 vya bunge vinavyohitajika kuunda serikali peke yao. Matokeo ya mwisho yanaweza kuchukua muda kwani bado wanaendelea kuhesabu idadi ya kura nyingi zilizopigwa kwa njia ya posta.

XS
SM
MD
LG