Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 13:30

Annan, Mkapa wakutana na viongozi wa mseto kenya


Kofi Annan (C), Raila Odinga (R) na mwendesha mashtaka wa zamani wa ICC Moreno Ocampo (L)
Kofi Annan (C), Raila Odinga (R) na mwendesha mashtaka wa zamani wa ICC Moreno Ocampo (L)

Viongozi hawa pamoja na wengine barani Afrika walisaidia kupatikana amani na kuundwa kwa serikali ya mseto baada ya ghasia za uchaguzi mkuu Kenya

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annan pamoja na Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa wapo nchini Kenya kwa muda wa siku nne kuchunguza mafanikio yaliyotekelezwa na serikali ya mseto tangu kuzuka kwa ghasia za uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2008.

Ziara hiyo pia inafuatia hali ya wasi wasi kuhusu uwezekano wa kutokea ghasia zaidi wakati wa uchaguzi wa rais na wabunge unaotarajiwa kufanyika mwezi machi mwakani.

Viongozi hao wanashauriana na maafisa wakuu wa serikali ya Kenya, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi muhimu za taifa kuhusu mabadiliko muhimu yaliyotekelezwa na serikali ya mpito kabla ya uchaguzi mkuu. Pia bwana Annan na bwana Mkapa watakutana na viongozi wa kidini, wafanyabiashara, wanahabari na jumuiya ya kimataifa.

Bwana Kofi Annan, Benjamin Mkapa, bibi, Craca Machel pamoja na viongozi wengine kadhaa wa bara la Afrika walisaidia kwa kiwango kikubwa kusitisha ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya ambapo zaidi ya watu 1,000 waliuwawa na maelfu kukoseshwa makazi. Serikali ya mseto nchini Kenya itamaliza muda wake mara tu baada ya uchaguzi mkuu ujao.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:55 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
XS
SM
MD
LG