Shirika la habari la serikali la Angop limeripoti kuwa waziri Diamantino de Azevedo, ametoa tangazo hilo kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri, ukiongozwa na rais Joao Laurenco.
Baada ya tangazo hilo, Azevedo amewaambia wanahabari kwamba, “ Tunahisi kwamba kwa sasa Angola hainufaiki kwa kubaki kwenye shirika hilo, na kwa ajili ya maslahi yake, imeamua kujiondoa.”
Ripoti za vyombo vya habari zinasema kwamba huenda hatua hiyo imetokana na uamuzi wa OPEC mwezi uliopita wa kushusha kiwango cha mgao wa mafuta kwa Angola mwaka ujao hadi mapipa milioni 1.11 kwa siku, hatua ambayo haikubaliani nayo.
Inasemekana kwamba waziri huyo aliandikia OPEC barua ya kupinga hatua hiyo. Data iliyotolewa awali inaonyesha kwamba kufikia Oktoba, Angola ilikuwa inazalisha takriban mapipa milioni 1.6 ya mafuta kila siku.
Forum