Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 21:17

Merkel aanza mazungumzo ya kuunda serikali


Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Chama cha The Alternative for German kimeahidi kutumia jukwaa lake katika bunge kuirejesha nchi na watu wake. Chama cha AFD kilishinda takribani asilimia 14 ya kura katika uchaguzi wa Jumapili na kupata viti 94.

Chama cha Christian Democrats cha Chansela Angela Merkel kilishinda idadi kubwa ya kura lakini kilipata wingi wa chini katika miaka 70. Merkel ameanza mazungumzo na vyama vingine kujaribu kuunda serikali utaratibu ambao utaweza kuchukua miezi kadhaa.

Wengi wanaamini mvutano wa karne ya 20 uliipatia kinga Ujerumani kutorudi kwenye siasa za mrengo wa kulia. Matokeo ya uchaguzi wa Jumapili yalithibitisha hilo si sahihi.

Kwa wapinzani wake ambao walikusanyika kupinga matokeo mjini Berlin ajenda ya kupinga wahamiaji ya chama cha The Alternative For German inafanana na kuongezeka madaraka ya NAZI.

Makundi ya wayahudi yalikuwa miongoni mwa wale wanaoelezea khofu kwa matokeo.

Alexander Gauland (R) akiwa na Alice Weidel
Alexander Gauland (R) akiwa na Alice Weidel

Kiongozi mwenza wa AFD, Alexander Gauland, aliwahi kusema wajerumani wanatakiwa kujivunia mafanikio ya jeshi lao katika vita ya pili ya dunia. Kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumatatu alikanusha kwamba chama ni cha ubaguzi wa rangi.

“Gauland alisema hakuna kitu chochote katika chama, katika program yake ambapo itaweza au inaonekana kuwasumbua wayahudi wanaoishi hapa Ujerumani. Alisema ahadi yake ya kuirejesha nchi ni ishara tu anaongeza kwamba hataki kuipoteza Ujerumani kuvamiwa na wageni kutoka tamaduni za nje hivyo ndivyo inavyomaanisha”.

Mchambuzi Profesa Tanja Borzel wa Free University mjini Berlin anasema uamuzi wa Chansela Merkel kuwaruhusu wahamiaji karibu milioni moja kuingia Ujerumani wakati wa mzozo mkubwa wa wahamiaji na wakimbizi mwaka 2015 kumepelekea wengi kumuadhibu kwenye upigaji kura.

“Watu wengi ambao walipiga kura kwa Alternative For Germany hawakupiga kura kwenye chama kwa sababu wanashirikiana mtazamo. Ni dhahiri ilikuwa ni kura ya kupinga’’.

Mafanikio ya mrengo wa kulia yamefunika ushindi wa Merkel ambao unampa muhula wanne madarakani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG